Skip to main content

BARUA KWA WILLIAM RUTO by Mohammed Ali

Hujambo bwana kusema na kutenda. Naomba safari hii kabla hujatenda nikujulishe mawili hivi. Najua huna raha, hupati usingizi na unahofia maisha yako licha ya utajiri uliyonayo. Leo hii umejipata kubanwa na uliowaamini. Ndoa za haraka na tama zina shida bwana Ruto. Ukipenda viazi usiogope mimba ndio msemo wetu kule vilima vya raha. Ndoa yako na Uhuru Kenyatta imefikia kiwango cha mtu mmoja kati yenu kupata mimba. Si mimba ya mtoto bali mimba ya machungu na kusalitiana. Miaka ya nyuma kabla ya wewe kuwa HUSTLER wa kizazi kipya niliwahi


kukutembelea mara kwa mara katika afisi zako katika jumba la Transnational. Tulizungumza na kutaniana na hata kuzungumza kwa simu. Ulikuwa machachari na mtu wa watu. Mwaka wa 2007/ 2008 baada ya ghasia za baada ya uchaguzi wewe na Raila mlikuwa chanda na pete mkijaribu kuunda serikali ya muungano na kupigania nafasi ya ukubwa wa wana odm katika serikali hiyo iliyowaibia kura. Katika pilka pilka hizo usaliti wa hali ya juu ulitendeka.

Wabakaji wa demokrasia walianza kunoa kisu huku nyinyi mkidhani mambo yalikuwa yashakwisha. Baada ya kufanyiwa unyama na PNU nilidhani mmejifunza mawili kuhusiana na ndoa za kipumbavu. Lakini naona mlisahau kuwa
ukila na kipofu kuwa mwangalifu kwani akikosa nyama atakushika mkono. Sasa nahofia chakula cha jubilee kimeisha na vipofu wote wanataka kukushika wewe mkono uwe kitoweo chao cha mwisho. Hamna anayekupenda, wewe ulikuwa chombo, chombo cha kuwavukisha wao kutoka masaibu yao. Kila mwenda kwa mganga lazima atoe kafara na kafara ni wewe. Nahofia utafungwa ama utakuwa mkimbizi wa ndani kwa ndani na ndio hio siku utajua masaibu ya kuishi kama wakimbizi wa ndani kwa ndani mwaka wa 2007/8. Utakuwa huna raha, utadhalilishwa, utakuwa mnyonge bila haki na hatimaye utakuwa huna maana kwa serikali ya TNA. Wacha niseme TNA kwa sababu URP haina usemi tena. URP imebakwa peupe wazi wazi, URP inalea mimba haramu, mimba ya kujitakia.


William Ruto usidanganywe na maombi za kinafiki zinazotekelezwa na wafuasi na maadui wako. Kama unataka kutatua shida zako binafsi na maombi tasa pole. Maombi ni ya kuondoa usinzi, wanaofumaniwa na wake za watu, mapepo na kumshukuru mungu na kumwogopa. Sio safari za mahakamani. Ruto, imefika wakati wa kucheza karata yako ya mwisho. Katika kucheza kwako jiepushe na Adan Duale na Kipchumba Murkomen hawa wawili ni wajuzi wa ligi za kitoto au wacha niseme ligi za mchezo wa tufe( mpira wa karatasi) unaochezwa na watoto. Hawatokusaidia ila watazidi kuongeza kuni kwenye moto. Moses Kuria anafanya yanayofanywa na Duale na Kipchumba ndani ya TNA sasa moto umewaka na ni sharti chakula kipikwe.

Kabla wakupike janjaruka. Kenya imekuwa taifa la kuzalisha wanafiki na watu waoga. Tumekubali ukiritimba itawale. Profesa hana tofauti na mtoto wa darasa la kwanza. Jiepushe na wanaokuzunguka na kujifanya wasomi ila ni watu wa maslahi. Maji tayari yamemwagika lakini ni wewe kuamua mkondo wa maji hayo. Huna budi kurudi kwa marafiki zako wa zamani kwani tayari wakenya washajua kikulacho ki nguoni mwako. Kwa maoni yangu binafsi na naomba unikosoe ni wewe kujiondoa mara moja kwenye muungano wa kinafiki. Warudie uliowakosea na uombe msamaha hakika Mungu anatuamrisha kuwasamehe maadui. Najua ni aibu kwako lakini kumbuka una familia. Aidha usiwahi kuwaona ama uishi bila ya kuwaona. Uamuzi umo mikononi mwako. Kuna uwezekano wa kujifunza na haya na kuamua kuunda muungano wa ukombozi wa tatu kina nyinyi mkiwa nyuma muwaachie vijana usukani. Kuna ile kadi moja ya mwisho ya wewe kuwatumia wana URP kupasisha mswaada na wana CORD wa kumwondoa Uhuru Kenyatta mamlakani kwa wingi wa kura bungeni lakini kwa yale umewafanyia wakenya miaka mitatu sioni kama CORD itakubali uwe Rais kwa miaka miwili iliyosalia kwa mujibu wa katiba ya Kenya. Bwana Ruto huu ni wakati wako wakuwaza na kuwazua. Tunazo changamatoto zinazotukabili kama taifa. Badala ya kukaa na kujiuliza kwa nini tuko hapa na tutatoka vipi, tunakaa na kuongea mambo ya kinafiki na ukabila. Akili ndogo kutawala akili kubwa. Watu wenye akili kubwa wanaweka akili zao mfukoni kwa sababu ya ushabiki wa kivyama badala ya kukaa na kutatua matatizo ya wakenya. Bunge limekuwa bunge la kitototo. Wakenya sasa wanataka bunge la mapinduzi. Badala ya kuwazomea wakenya waskilizeni.


Deni la Kenya linazidi kuongezeka. Kila mkenya anadaiwa hata mimba inadaiwa. Ndio taifa tuliyonayo sasa. Williama Samoei Arap Ruto huna la ziada sasa. Tayari chama chako na uongozi wako umebakwa ki-demokrasia. Waswahili wanasema mimba ya mwanaharamu huingia mara moja ya pili ni kusudi. Je, ulisahau mimba ya mwaka wa 2007? Kwa nini umekubali mimba nyengine mwaka wa 2013? Umechezewa shere tangu na mwanzo wa ndoa yenu ya vichochoroni. Huna sura sasa, wakenya hawatokukubali tangu watoto wao wapigwe na vitoa machozi wakipigania uwanja wa shule yao ya msingi wa langata. Huna sura tena, ufisadi umekuwa jina lako la pili. Wakenya hawakuamini tena. Iwapo ulijikakamua na kuwasaidia wakenya tangu mchukue uongozi leo hii wangekusitiri na kukupokea lakini ulisahau kuna kupanda na kushuka. Leo zamu ya kushuka kukutana na sisi kina yahe. Hatutakudhulumu wala kukuita majina, sisi tutaoongozwa na dini na hekima.

Karibu nyumbani lakini kumbuka sisi hatuna nguvu za kukusaidia maana sote ni maskini kama mlivyotufanyia mlipokuwa masimba. Mlitufanya maskini kwa kutudhulumu na uongozi wenu wa kusema na kuenda. Leo bwana Ruto hakuendeki. Huna budi kumkumbatia Raila Amollo Odinga na kumwomba msamaha kwa semi zako za chuki dhidi yake. Akufaye kwa dhiki ndiye rafiki. Kumbuke hata simba ni mkali lakini hutiwa mimba. Kuwa na ijumaa njema. Ni mimi rafiki wako wa zamani, Mohammed Ali.
Mohammed Ali ni Mhariri Mkuu wa Kitengo cha Upekuzi KTN.

Kuwasiliana naye:

mali@standardmedia.co.ke,

FB: Official Jicho Pevu with Mohammed Ali,

Twitter: @mohajichopevu


TWAOMBA RADHI.
Katika makala ya wiki iliyopita ( kuna serikali kweli Kenya ), tulisema kuwa tangu jubilee iingie mamlakani, wakenya zaidi ya laki tatu wamepoteza maisha yao kutokana na hali mbaya ya usalama. Tungelipenda kusahihisha na kusema kuwa tulikuwa tukimaanisha watu zaidi ya 300.




>>>>..link >>> https://www.facebook.com/Official.JichoPevu/posts/1050381778346741


Comments

Popular posts from this blog

There is no regret in Obedience

It’s a guarantee your life will never be the same again when you obey God. God is our CREATOR and our DIRECTOR meaning he knows the best way for our lives since he loves us, our role is to simply OBEY Him. Obedience is everything when we are relating to God. Obedience is the KEY ingredient in the kingdom of God. God is always ready to manifest himself in our lives when we obey Him and his word(John 14:23 Jesus Replied, “Anyone who loves me will obey my teaching. My Father will love them, and we will come to them and make our home with them.” Like 5:5 Simon Peter an experienced fisherman with a fishing business had toiled the whole night without any catch of fish and he was frustrated and tired and he was washing his nets UNTIL Jesus told him to Launch out into the deep again. Peter had a CHOICE to say YES or NO but he choose to OBEY and he said: “Nevertheless AT THY WORD I WILL LET DOWN THE NET”. The moment he chooses to obey instead of Questioning, Analyzing and trying ...

President Uhuru Kenyatta sets ablaze world's biggest Ivory Pile #WorthMoreAlive #IvoryBurn

Kenya has burned more than Sh31 billion worth of ivory in a bold sign of commitment to declaring a war on ivory trade and poaching. President Uhuru Kenyatta on Saturday lit fire on the 105 tonnes of ivory, stack up in 11 huge pyramid-shaped pyres, that is expected to burn for at least three days. Speaking at the burning ceremony, President Kenyatta said Kenya will not tolerate ivory trade even as the country has to grapple with “a new generation of poachers with sophisticated weapons who are threatening national heritage and safety of communities.” By destroying the ivory, we declare once and for all that our National Heritage is not for sale. For us ivory is worthless, unless it is on our elephants said the president Check the pictures below:>>>>>

CA sounds alert on fake software

The telecommunications sector watchdog has warned companies and individual Internet users from buying fake software, saying it now offers hackers the most common loophole for executing cyber-attacks. The Communications Authority of Kenya (CA), through the National Computer Incident Response Team Co-ordination Centre (National KE-CIRT/CC), warned on Thursday that cybercriminals have changed tack and are now using third-party software to deliver threats to unsuspecting users in an attempt to compromise and steal their personal data. “Though Kenya has not been adversely affected by such attacks as at now, the trend depicts a serious concern in cybercrime management and thus a precaution should be taken when dealing with outsourced products and personnel,” said acting CA director- general Christopher Kemei in a statement. Kenyan businesses lose billions of shillings and troves of sensitive information to hackers every year. SOURCE